Akiwa Waziri wa Afya, Mh. Pandu A. Pasua alihusika katika kutoa idhini ua uingizwaji nchini wa dawa feki za Malaria ulioua zaidi ya watanzania 3,000. Blogu ya Jicho la Tatu limefanikiwa kupata ushahidi mpya ambao unaonyesha kwamba Mh. Pandu A. Pasua alifanikisha mpango wa uingizwaji wa madawa hayo kwa maslahi binafsi na kusababisha maafa kwa Taifa.
Vyanzo vyeti vya habari vinaonyesha kuwa taarifa za awali za uingizwaji wa madawa hayo ulipingwa na kukataliwa vikali na hayati Sereli Mushi ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na dawa lakini pamoja na jitihada za taasisi hiyo kuzuia uingizwaji huo Mh. Pandu alitumia nafasi yake akiwa waziri kuingiza madawa hayo.
Katika barua iliyonaswa na Blogu ya Jicho la tatu yenye kumbukumbu namba Gov/WAF/TCD/578/3/7/2004 iliyosainiwa na Mh. Pandu kwenda kwa Taasisi ya Chakula na dawa inaonyesha kuwa Mh. Pandu aliharakisha mchakato wa uingizwaji wa madawa hayo na kuamuru usambazwaji wa haraka wa dawa hizo kwenda katika hospitali za Umma hata baada ya kupokea taadhari kutoka kwa taasisi hiyo
kama inavyokumbukwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kipindi hicho Mh. Dr. Maneno Muta Mkangwa akizungumzia suala la kashfa ya malaria Bungeni alitanabaisha kuwa vielelezo vilivyoambatanishwa na katibu mkuu wa wizara ya Afya kipindi hicho Mama Zuhura Odemba vilikinzana na ushahidi wa Mh. Pandu A. Pasua uliopelekwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

No comments:
Post a Comment