JICHO LA TATU: UKWELI KUHUSU PANDU A. PASUA

Mwandishi Wetu

Saturday, October 17, 2015

UKWELI KUHUSU PANDU A. PASUA


Pandu A. Pasua ni mmoja kati ya wanasiaswa wakongwe katika historia ya Tanzania. Ni mmoja kati ya viongozi wanaoheshimika sana kutokana na kuitumikia nchi katika kipindi kirefu akishika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi katika Chama na Serikali. 

Blogu ya Jicho la tatu katika kipindi hiki muhimu cha kuelekea Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani imeona ni jambo muhimu katika mfululizo wa makala zinazohusu uchaguzi kutoa maelezo ya kina kuhusu wasifu wa Mh. Pandu A. Pasua ili watanzania hasa vijana waweze kufahamu mengi kuhusu viongozi wetu na mchango wao katika jamii.

Mh. Pandu A. Pasua alizaliwa tarehe 15/02/1948 huko Songea mkoani Ruvuma akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto sita ya Mzee Mkasi Ambani Pasua. Toka akiwa mdogo Pandu alionyesha uwezo mkubwa shuleni na hivyo kufanikiwa kupata ufadhili wa wamisionari wa kikatoliki katika shule ya Seminari ya Songea mjini.


kama ilivyokuwa kwa watanania waliofanikiwa kupata elimu kabla ya Uhuru, Mh. Pandu alipata nafasi ya kuendelea na masomo yake ya juu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam katika miaka ya ambapo alihitumu na Shahada ya Historia na Sayansi ya Siasa 

No comments:

Post a Comment